Nenda kwa yaliyomo

Andeoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngao ya Saint-Andéol-de-Clerguemort, ikimuonyesha Mt. Andeoli.

Andeoli (Smirna, leo nchini Uturuki, karne ya 2 - karibu na Viviers, 208) alikuwa Mkristo kutoka Smirna (leo nchini Uturuki) aliyefanya umisionari huko Galia Kusini (leo Ufaransa) hadi alipouawa wakati wa dhuluma ya kaisari Septimius Severus [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 1 Mei[2].

Akiwa shemasi, alitumwa na askofu wake Polikarpo,[3] kuinjilisha Galia pamoja na Beninyo wa Dijon.

Kati ya waliowaongoa, mmojawao ni Sinforiani wa Autun, baadaye mfiadini.

Andeoli aliendelea hadi eneo la Viviers alipouawa kwa upanga.[4]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.