Nenda kwa yaliyomo

Suez

Majiranukta: 29°58′N 32°33′E / 29.967°N 32.550°E / 29.967; 32.550
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bandari na chanzo cha mfereji mjini Suez

Suez (ar. السويس as-Suways) ni mji na bandari nchini Misri. Uko kwenye mwambao wa kaskazini wa ghuba ya Suez au, kwa lugha nyingine, upande wa kusini wa Mfereji wa Suez. Mwaka 2012 mji ulikuwa na wakazi 565,716.

Suez iko takriban kilomita 135 upande wa mashariki wa Kairo kwenye shingo ya nchi ambako umbali na Bahari ya Mediteranea haifikii kilomita 150. Kwa sababu hiyo Suez ilikuwa mahali palipofaa kwa biashara na masoko ya biashara kati ya Mediteranea na Bahari Hindi. Tangu kubuniwa kwa njia ya bahari kutoka Ulaya kwenda Uhindi kupitia Rasi ya Tumaini Jema (Afrika Kusini) biashara hiyo ilififia. Hata hivyo Suez iliendelea kuwa bandari ya maana kwa wasafiri Waislamu walioelekea Makka kwa hajj.

Umuhimu wa Suez ulirudishwa na kuongezwa tangu kujengwa kwa Mfereji wa Suez tarehe 17 Novemba 1869. Sehemu kubwa ya biashara ya dunia kwa meli ilipita kwenye mfereji na bandari ya Suez.

Suez imeendelea kuwa mji muhimu wa viwanda pamoja na vile vya kusafisha mafuta, vya kemia na feleji.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Suez kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


29°58′N 32°33′E / 29.967°N 32.550°E / 29.967; 32.550