Nenda kwa yaliyomo

Tito

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Tito askofu.
Kanisa lake huko Heraklion.

Tito (labda 12 - 107) ni mmojawapo kati ya viongozi wa kwanzakwanza wa Kanisa, akiwa mwenzi na mwandamizi wa Mtume Paulo, anayetajwa katika Nyaraka zake mbalimbali.

Alikuwa naye huko Antiokia akaongozana naye kwenye Mtaguso wa Yerusalemu,[1] ingawa jina lake halitajwi katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

Kabla hajabatizwa alikuwa Mpagani, hivyo Paulo alikataa kabisa dai la kwamba atahiriwe ili aokoke.

Kadiri ya Nyaraka, baadaye alikuwa naye Efeso, akatumwa Korintho.[2]

Walikutana tena Makedonia,[3] halafu akawa kisiwani Krete ili kuimarisha uongozi wa Kanisa la huko.[4]

Habari za mwisho ni kwamba alikwenda Dalmatia [5].

Agano Jipya halisimulii kifo chake.

Mapokeo yanasema Paulo alimpa daraja ya uaskofu kwa ajili ya Gortyn huko Krete, na kwamba alifariki mwaka 107, akiwa na umri wa miaka 95.

Tangu mwaka 1969, Kanisa Katoliki la Kilatini linamwadhimisha pamoja na Timotheo tarehe 26 Januari, siku inayofuata ile ya Uongofu wa Mt. Paulo, mwalimu wao.[6][7][8]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Wagalatia 2:1-3; Matendo 15:2
  2. 2 Korintho 8:6; 12:18
  3. 2 Korintho 7:6-15
  4. Tito 1:5
  5. https://www.santiebeati.it/dettaglio/22500
  6. Calendarium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 1969), uk. 116
  7. Martyrologium Romanum
  8. https://www.santiebeati.it/dettaglio/22475

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 33
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 27-28
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 20
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tito kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.