Nenda kwa yaliyomo

Udeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Udani)
Udeni
Danmark (Kideni)
Wimbo wa taifa: "Der er et yndigt land"
"Kong Christian stod ved højen mast" (Wimbo wa kifalme)
Udeni katika Ulaya
Mji mkuu
na mkubwa
Copenhagen
Lugha rasmiKideni
Kabila86.11% Wadeni
13.89% Wengine
 • Mfalme
Frederik X
 • Waziri Mkuu
Mette Frederiksen
 • Muungano
Karne ya 8
 • Katiba ya sasa
5 Juni 1849
Eneo
 • Jumlakm2 43,094 (ya 130)
 • Maji (asilimia)1.74%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2024 5,982,117
 • Msongamano138.8/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2024
 • Jumla $496.696 bilioni
 • Kwa kila mtu $83,454
PLT (Kawaida)Kadirio la 2024
 • Jumla $412.293 bilioni (ya 37)
 • Kwa kila mtu $69,273
HDI (2023) 0.962
juu sana
Gini (2022)27.7
SarafuKrona ya Udeni (DKK)
Majira ya saaUTC+1 (CET) / UTC+2 (CEST)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+45
Jina la kikoa.dk

Udeni ni nchi ya Kaskazini mwa Ulaya iliyoko katika eneo la Skandinavia. Inapakana na Ujerumani upande wa kusini, na inazungukwa na Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki. Ina idadi ya watu takriban milioni 5.9 (2024), na mji wake mkuu na mkubwa zaidi ni Copenhagen, ambao pia ni kitovu cha uchumi, biashara, na utamaduni. Udeni inajumuisha eneo la bara la Jutland pamoja na visiwa vya Zealand, Funen na visiwa vingine vidogo. Ina mamlaka ya ndani ya kujitawala ya Greenland na Visiwa vya Faroe. Inatambulika kwa ustawi wa kijamii, historia tajiri, upangaji bora wa miji, na mchango wake mkubwa katika utamaduni wa Nordic.

Udeni ina mfumo wa serikali wa kifalme wa kikatiba unaoendeshwa na bunge la aina moja linaloitwa Folketing. Mkuu wa nchi ni mfalme, lakini mamlaka ya kiutendaji iko mikononi mwa waziri mkuu na baraza la mawaziri. Ingawa ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Udeni imeamua kutotumia sarafu ya euro, na badala yake hutumia Kroni ya Kideni (DKK). Nchi hii huorodheshwa miongoni mwa mataifa yenye viwango vya juu vya maisha, elimu bora, huduma za afya zenye upatikanaji mpana, na ulinzi wa mazingira.Uchumi wake una msingi imara unaotegemea sekta kama vile nishati mbadala, viwanda vya dawa, usafirishaji wa baharini, na teknolojia ya kisasa.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Udeni ina eneo la km² 43.000. Theluthi ya eneo hili ni kwenye visiwa 443 vya Udeni ambavyo 76 tu kati yake vinakaliwa na watu.

Visiwa vikubwa ni Funen (Fyn), Zealand (Sjælland) na Bornholm (Bornholm).

Rasi ya Jutland ni sehemu kubwa ya eneo. Jutland ni Udeni bara. Ina urefu wa km 300 kuelekea kaskazini kutoka mpaka wa Ujerumani hadi ncha yake kwa Skagen.

Kwa jumla Udeni iko tambarare. Mwinuko wa juu una kimo wa m 170 pekee juu ya UB.

Kumbuka kwamba orodha hii inahusu Udeni tu kama nchi, si Visiwa vya Faroe na Greenland.[1][2] Mlima mrefu wa ufalme mzima ni Gunnbjørn, Greenland, m 3,700 juu ya UB.

No Mwinuko Sehemu ya Nchi Kimo
1. Møllehøj Skanderborg manisipaa 170,86 d
2. Yding Skovhøj Horsens manisipaa 170,77 d
3. Ejer Bavnehøj 170,35 d
4. Lindbjerg 170,08 d
5. Basi Margretelyst 169,78 d
6. Vistofte 169,44 d

Mpaka mwaka 1847 Himmelbjerget, Skanderborgs, m 147 ilifikiriwa kuwa mwinuko mkubwa wa Udeni.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza waliojulikana katika historia kwa jina ni makabila ya Wakimbri na Wateutonia waliohamia hadi Ulaya ya kusini wakati wa njaa mnamo mwaka 113 KK.

Katika karne ya 8 hadi karne ya 11 BK majambazi wa baharini kutoka Udeni na Norway waliogopwa kote Ulaya kwa jina la "Waviking". Walivamia pia Uingereza mara kwa mara na kujenga makao huko. Tangu mwaka 793 walitawala eneo la Danelag (au: Danelaw) kaskazini na kaskazini-mashariki mwa Uingereza wa leo.

Katika karne ya 8 na karne ya 10 maeneo madogo yaliunganishwa. Wafalme wa kwanza wanaojulikana kutawala Udeni yote walikuwa Garm Mzee na Harald Jino Buluu (mnamo mwaka 980). Harald alikuwa mfalme wa kwanza wa kupokea Ukristo wa Kanisa Katoliki.

Udeni ikawa nchi yenye nguvu katika Skandinavia na kwenye pwani za Baltiki.

Kuanzia 1397 hadi 1521 nchi zote za Skandinavia ziliunganishwa katika maungano ya kifalme chini ya wafalme wa Udeni ilhali kila nchi ilijitawala katika mambo ya ndani.

Baada ya Uswidi kujitenga na umoja huo, Norway iliendela kuwa chini ya Udeni hadi mwaka 1814.

Mwaka 1537 Udeni ilijiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na Kanisa la Kilutheri likawa dini rasmi nchini hadi leo, ikifuatwa na 76.9% za wakazi. Udeni ilikuwa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri, lakini leo 3% tu wanashiriki ibada ya Jumapili.

Baada ya vita za Napoleoni Udeni iliondolewa utawala wa Norway iliyounganishwa na Uswidi mwaka 1814. Lakini makoloni ya Greenland, Iceland, Faroe na visiwa vya Karibi zilibaki chini yake.

Karne ya 19 ilileta fitina na Ujerumani juu ya utawala wa Schleswig na Holstein. Baada ya vita ya 1864 Udeni ilipaswa kuacha majimbo hayo mawili kwa Ujerumani.

Udeni haikushiriki katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza lakini ilirudishwa sehemu ya kaskazini ya jimbo la Schleswig.

Wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Pili Udeni ilivamiwa na Ujerumani mwaka 1940 hadi 1945. Wakati wa vita Iceland iliamua kutangaza uhuru wake.

Mwaka 1948 mara baada ya vita visiwa vya Faroe vilipewa madaraka ya kujitawala lakini vilibaki ndani ya umoja na Udeni. Koloni la Greenland lilipewa madaraka hayo mwaka 1979.

Udeni ikawa kati ya nchi zilizounda UM na pia NATO.

Mwaka 1973 ikajiunga na Jumuiya ya Ulaya (sasa: Umoja wa Ulaya), lakini imekataa kutumia euro badala ya krona.

Kutokana na uzazi mdogo, miaka ya mwisho uhamiaji umeongezeka, hivi 12.3% wana asili ya kigeni (yaani hata mzazi wao mmoja ni raia na mzaliwa wa Udeni).

Mnamo Septemba 2024, wakazi walikuwa 5,982,117. Kati yao, Wadeni asili ni 88,67%. Wengine ni wahamiaji (kutoka Uturuki, Polandi, Syria, Ujerumani, Iraq, Romania, Lebanoni, Pakistan, Bosnia na Herzegovina, Somalia n.k.) au wamezaliwa na mhamiaji walau mmoja.

Lugha ya nchi ni Kideni, jamii ya Kijerumaniki, na 86% za wakazi huongea vizuri Kiingereza kama lugha ya pili.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, lakini 3% tu wanashiriki ibada ya Jumapili na 19% tu wanaona dini ni muhimu maishani. Dini rasmi ni Kanisa la Udeni (la Kilutheri; 71.2%). Wakatoliki hawafikii 1%. Kutokana na uhamiaji, Waislamu ni 4.4%.

Watu maarufu

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "kort & Matrikelstyrelsen, nyt højeste punkt i Danmark". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-10. Iliwekwa mnamo 2017-11-07.
  2. Faktoider.nu, Danmarks högsta punkt
  • (Kidenmark) Busck, Steen and Poulsen, Henning (ed.), "Danmarks historie  – i grundtræk", Aarhus Universitetsforlag, 2002, ISBN 87-7288-941-1
  • (Kidenmark) Gammelgaard, Frederik; Sørensen, Niels (1998). Danmark – en demokratisk stat. Alinea. ISBN 87-23-00280-8. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • (Kidenmark) Jørgensen, Gitte (1995). Sådan styres Danmark. Flachs. ISBN 87-7826-031-0. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • (Kidenmark) Michaelsen, Karsten Kjer, "Politikens bog om Danmarks oldtid", Politikens Forlag (1. bogklubudgave), 2002, ISBN 87-00-69328-6
  • (Kiswidi) Nationalencyklopedin, vol. 4, Bokförlaget Bra Böcker, 2000, ISBN 91-7024-619-X.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Ramani
Biashara
Vyombo vya habari
Mengineyo
  • Vifanord.de – library of scientific information on the Nordic and Baltic countries.


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Udeni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.