Iraki
Jamhuri ya Iraki جُمْهُورِيَّة ٱلْعِرَاق Jumhūriyyat al-ʿIrāq (Kiarabu) کۆماری عێراق Komarî Êraq (Kikurdi) | |
---|---|
Wimbo wa taifa: مَوْطِنِيْ Mawṭinī ("Nchi Yangu") | |
Mji mkuu na mkubwa | Baghdad |
Lugha rasmi | Kiarabu, Kikurdi |
Lugha ya taifa | Kiasiria, Kifarsi, Kituruki, Kiarmenia (kikanda) |
• Rais | Abdul Latif Rashid |
Mohammed Shia Al Sudani | |
Historia | |
3 Oktoba 1932 | |
• Kutangazwa kwa Jamhuri | 14 Julai 1958 |
• Katiba ya sasa | 15 Oktoba 2005 |
Eneo | |
• Jumla | km2 438,317 (ya 58) |
• Maji (asilimia) | 4.93% |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2025 | 47,020,774 |
• Msongamano | 82.7/km2 |
PLT (PPP) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $655.417 bilioni |
• Kwa kila mtu | ▲ $14,757 |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $264.149 bilioni (ya 46) |
• Kwa kila mtu | ▲ $5,947 |
HDI (2023) | ▲ 0.695 kati |
Gini (2012) | 29.5 |
Sarafu | Dinar ya Iraki (IQD) |
Majira ya saa | UTC+3 (AST) |
Upande wa magari | Kushoto |
Msimbo wa simu | +964 |
Jina la kikoa | .iq .العراق |

Iraki (jina rasmi: Jamhuri ya Iraki; kwa Kiarabu: العراق) ni nchi ya iliyoko katika Asia ya Magharibi. Inapakana na Uturuki kaskazini, Iran mashariki, Kuwaiti na Ghuba ya Uajemi kusini, Saudi Arabia kusini magharibi, Jordan magharibi, na Syria kaskazini magharibi. Iraki ina eneo la takriban kilomita za mraba 437,072, na kwa makadirio ya mwaka 2024, idadi ya watu imefikia takriban milioni 45.Mji mkuu wa Iraki ni Baghdad, ambao ulikuwa mojawapo ya vituo muhimu vya kielimu na kitamaduni katika enzi za Dola ya Kiislamu ya Abbasiyya.
Iraki ina utajiri mkubwa wa mafuta, jambo lililoifanya kuwa nchi muhimu kiuchumi katika eneo la Mashariki ya Kati. Hata hivyo, historia ya hivi karibuni imekuwa na changamoto, ikijumuisha vita vya ndani, uvamizi wa Marekani mwaka 2003, na ghasia zilizosababishwa na makundi ya kigaidi kama vile Dola la Kiislamu (ISIS).
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Sehemu kubwa ya Iraq ni jangwa lakini kuna eneo lenye rutuba kati ya mito ya Frati na Hidekeli.
Kaskazini ni hasa nchi ya milima inayopanda hadi ya kimo cha m 3,611 juu ya UB.
Hali ya hewa inalingana na mazingira. Kipindi cha kiangazi kuna joto kali. Majira ya Desemba-Februari kuna halijoto ya kupoa kusini na baridi kali mlimani.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Iraq ni nchi yenye historia ndefuː ilikuwa kitovu cha ustaarabu wa binadamu, mahali pa miji ya kwanza duniani katika Sumeri na Babeli.
Baada ya kusambaratika kwa milki ya Waturuki Waosmani walioitawala muda mrefu, Iraq ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mataifa mwaka 1932 ingawa hali halisi ilikuwa nchi lindwa chini ya athira ya Uingereza hadi mwaka 1958.
Miaka ya hivi karibuni imejulikana hasa kutokana na vita mbalimbaliː kwanza vita dhidi ya Uajemi chini ya serikali ya Saddam Hussein tangu 1981, baadaye vita dhidi ya Kuwait na Marekani.
Vita vya pili vya ghuba ya 2003 iliyoleta uvamizi wa Marekani ilizidi kuleta vifo na uharibifu.
Hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoingiliwa na DAESH iliyoteka sehemu kubwa ya nchi, hasa kaskazini na magharibi, hadi mwishoni mwa mwaka 2017.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Lugha rasmi na ya kwanza ni Kiarabu, ikifuatwa na Kikurdi ambayo pia imekuwa lugha rasmi, halafu lugha nyingine za jamii mbalimbali ambazo pengine zinatambulika kieneo.
Wakazi wengi (95%), hasa baada ya vita vya hivi karibuni, ni Waislamu, wakiwemo kwanza Washia halafu na Wasuni. Wakristo waliobaki ni 5%, wakiwemo hasa waamini wa Kanisa Katoliki la Wakaldayo na Waashuru wa Kanisa la Mashariki.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Iraq ina akiba kubwa za mafuta ya petroli ardhini. Mapato kutokana na mafuta yalileta maendeleo makubwa nchini hadi mwanzo wa kipindi cha vita vilivyoharibu sana nchi pamoja na uchumi wake.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Shadid, Anthony 2005. Night Draws Near. Henry Holt and Co., NY, U.S. ISBN 0-8050-7602-6
- Hanna Batatu, "The Old Social Classes and the Revolutionary Movements of Iraq", Princeton: Princeton University Press, 1978
- Charles Glass, "The Northern Front: A Wartime Diary"' Saqi Books, London, 2004, ISBN 0-86356-770-3
- A Dweller in Mesopotamia Ilihifadhiwa 25 Mei 2005 kwenye Wayback Machine., being the adventures of an official artist in the garden of Eden, by Donald Maxwell, 1921. (a searchable facsimile at the University of Georgia Libraries; DjVu & layered PDF Ilihifadhiwa 6 Septemba 2005 kwenye Wayback Machine. format)
- By Desert Ways to Baghdad Ilihifadhiwa 2 Aprili 2005 kwenye Wayback Machine., by Louisa Jebb (Mrs. Roland Wilkins) With illustrations and a map, 1908 (1909 ed). (a searchable facsimile at the University of Georgia Libraries; DjVu & layered PDF Ilihifadhiwa 6 Septemba 2005 kwenye Wayback Machine. format)
- "Iraqi Constitution" (PDF). Ministry of Interior – General Directorate For Nationality. 2006-01-30. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-11-28. Iliwekwa mnamo 18 Februari 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Benjamin Busch, "'Today is Better than Tomorrow'. A Marine returns to a divided Iraq", Harper's Magazine, October 2014, pp. 29–44.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Serikali
- Presidency of Iraq Ilihifadhiwa 2 Julai 2014 kwenye Wayback Machine.
- Cabinet of Iraq Ilihifadhiwa 25 Oktoba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Taarifa za jumla
- Iraq entry at The World Factbook
- Iraki katika Open Directory Project
- Iraq profile from the BBC News
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Iraki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |