Vilogu
Mandhari
Vilogu (kwa Kiingereza: vlog) ni aina ya blogu ambayo huwa mbinu yake ya uwasilishaji wa jumbe ni kwa kutumia video. Kwa mapana, vilogu ni blogu ya video (video blog). Kwa wengi, video zao huwekwa kwa wavuti ya Youtube ambayo ndiyo iliyo na video nyingi sana.
Historia ya vilogu
[hariri | hariri chanzo]Msanii Nelson Sullivan alijulikana kwa kurekodi kazi yake na kuiwasilisha kwa watu kwa kutumia vilogu. Kazi yake aliiweza kurekodi katika miji tofauti kama vile New York.
Vilogu za kisasa
[hariri | hariri chanzo]Vilogu zilipata umaarufu sana mwaka 2005. Leo, ni watu wengi walio na vilogu zinazowasilisha jumbe tofauti kutoka masomo ya kupika, hisabati, uchumi, malezi, urembo na hata afya njema ya mwili.
Unachohitaji ili kuwa na vilogu
[hariri | hariri chanzo]- Hadhira ya kuwasilishia jumbe zako
- Uzoefu wa kuweka video
- Kamera nzuri ya kuchukua video pamoja na tripodi ya vilogu ya kusaidia kuchukua video zako
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |