Nenda kwa yaliyomo

Elizabeth II

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malkia Elizabeth II
Malkia Elizabeth II mwaka 2015
AmezaliwaElizabeth Alexandra Mary Windsor
21 Aprili 1926
Mayfair, London, Ufalme wa Muungano
Amekufa8 Septemba 2022 (miaka 96)
Kasri la Balmoral, Uskoti
Kazi yakeMtawala wa kifalme
NdoaPrince Philip, Duke wa Edinburgh (ndoa: 1947–2021)
WatotoWatoto 4, wakiwemo Mfalme Charles III, Princess Anne, Prince Andrew, na Prince Edward
WazaziMfalme George VI
Malkia Elizabeth , Malkia Mkuu
Elizabeth II mwaka 2006.

Elizabeth II alikuwa malkia wa Ufalme wa Muungano wa Britania (Uingereza na Welisi na Uskoti) na Eire Kaskazini) na malkia wa Milki ya Uingereza tangu mwaka 1952 hadi kufariki dunia tarehe 8 Septemba 2022. Alikuwa malkia kwa miaka 70 na siku 214. Katika historia yote ya dunia wako watawala wachache waliodumu madarakani muda mrefu kuliko yeye[1][2]. Soma zaidi wasifu wake hapa Anafuatwa na mwana wake wa kwanza, Charles III wa Uingereza.

Alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor mjini London tarehe 21 Aprili 1926 kama mtoto wa kwanza wa mfalme George VI wa Uingereza na Elizabeth Bowes-Lyon.

Alitangazwa kuwa malkia tarehe 6 Februari 1952 mara moja baada ya kifo cha baba yake George VI. Wakati ule alikuwa akitembelea Kenya iliyokuwa bado koloni la Uingereza akatembelea milima ya Aberdare.

Alipokea taji katika ibada rasmi tarehe 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey.

Kama mkuu wa Jumuiya ya Madola alikuwa pia mkuu wa dola wa nchi zifuatazo ndani ya jumuiya hii[3]:

Katika nchi zote aliposhika cheo hakuwa na mamlaka ya kiserikali ila alitawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.

Marejeo

  1. Queen Elizabeth II dies aged 96 Guardian (UK), 08.09.2022
  2. Mfalme Louis XIV wa Ufaransa alitawala miaka 72 kutoka 1643 - 1715; orodha hii inaonyesha wengine
  3. mbali ya nyingine ambazo katikati waligeuka Jamhuri
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elizabeth II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.